WASTARA: NATAKA KUOLEWA NA BILIONEA
IKIWA ni takribani mwaka mmoja tangu alipoondokewa na mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema sasa yupo tayari kuolewa lakini sharti la kwanza la muoaji lazima awe mtu mwenye fedha zake.Akizungumza na mwandishi , wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Wastara alisema, amekuwa mpweke kwa muda mrefu na sasa ni wakati muafaka wa kumpata mtu wa kuziba pengo la marehemu mume wake.
“Natamani kuolewa na bilionea. Najua nikiwa na mwanaume wa aina hiyo sitateseka, nitapata kila ninachokitaka. Unajua mimi kama mwanamke nina mambo mengi. Siyo siri natamani itokee siku moja niendeshe Hummer au Prado (aina za magari) kulingana na hadhi yangu.
0 comments: