Hapa akiwa muhimbili Baada ya kupata huduma ya matibabu, haya ni baadhi ya majeraha aliyoyapata
Joseph Yona akiingizwa katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI).Picha Zote na Global Publishers
----
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
![](//4.bp.blogspot.com/-pUImKMVPjCU/UswwsF1pUiI/AAAAAAACln4/TwvFZYGIiDE/s1600/8-chadema.jpg)
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko taarifa za tukio
la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya
Temeke, Josephat Yona Patrick.
Chama kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano, mbali ya kukemea kwa
nguvu zote tukio hilo la kihuni na mengine ya namna hiyo yenye lengo ya
ukatili dhidi ya binadamu, katika hatua ya sasa kinapenda kusema
yafuatayo juu ya tukio hilo ovu ;
1. Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi juu ya tukio hilo la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke ili
ukweli ujulikane na haki itendeke, kwa sheria kuchukua mkondo wake.
2. Chama kinawataka wanachama na Watanzania kwa ujumla kutulia,
hasa pale ambapo watu wenye hila na malengo yao, wanaanza kukihusisha
chama na tukio hilo. Watambue kuwa pamoja na mtu yeyote kuwa kiongozi wa
chama, bado anayo maisha yake na uhusiano na watu wengine katika jamii.
3. Jeshi la Polisi linapaswa kuyachukulia uzito mkubwa na
unaostahili matukio ya namna hii ambayo yanaanza kuota mizizi kutokana
na watu waovu wanayoyatekeleza kutochukuliwa hatua za kisheria ambazo
zingesaidia kuzuia yasitokee tena.
4. Watanzania bado wanakumbuka kwamba hadi sasa Jeshi la Polisi
limeshindwa kutoa taarifa za kina na kuchukua hatua za kisheria ambazo
zingesaidia ukweli kujulikana na haki kutendeka katika matukio ya
kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa madaktari Dk. Steven Ulimboka na
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda. Hivyo ingesaidia
kuzuia matukio mengine kutokea.
5. Ni kutokana na jeshi hilo kushindwa kuwajibika ipasavyo katika
matukio mengine ya namna hiyo, watu waovu wanaweza kutumia mwanya wa
kinachoendelea ndani ya CHADEMA kwa chama kuchukua hatua za kinidhamu
dhidi ya wanachama wasio waadilifu, kufanya matukio ya namna hiyo iii
kujenga taswira ya kukihusisha chama na uhuni huo unaobeba kila sifa ya
kuitwa ukatili dhidi ya binadamu.
6. Aidha kushindwa kwa Jeshi la Polisi kuwajibika ipasavyo katika
kufanya uchunguzi wa matukio hayo (yaliyotolewa kama mfano hapo juu) na
mengine ya namna hiyo, jeshi hilo linazidi kujiweka katika wakati mgumu
wa kukwepa tuhuma za baadhi ya watendaji wake kujua na kushiriki
masuala haya, hususan kwa kurejea tukio la kutekwa kwa Dkt. Ulimboka.
Imetolewa leo Jumanne, Januari 7, 2014 na;
Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
0 comments: