DEC12
MWENYETI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe
----
MWENYETI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amewataka wanachama wa chama hicho wamuulize Mbunge Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe wapi alikomtoa hadi kufikia ngazi na hadhi aliyonayo sasa katika medani ya siasa nchini.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika kongamano la miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Chaso) kwa kushirikiana na Baraza la Vijana la Chama hicho (BAVICHA)
Katika kongamano hilo lililofanyika katika Hoteli ya Land Mark, Mbowe ambaye alianza kwa kutaja historia yake kama mwasisi kijana wa CHADEMA na mwenyekiti wa kwanza, alisema mwaka 2003 akiwa katika harakati za kukijenga chama, alipita katika vyuo mbalimbali ili kupata vijana wasomi wajiunge na CHADEMA na ndipo alipompata Zitto, akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Nikiwa katika harakati zangu za kukijenga chama, nilipita Chuo Kikuu cha Dar es Salaam …nilibahatika kuwapata kina John Mrema, Halima Mdee, Zitto Kabwe, John Mnyika wakiwa viongozi ambao walipenda siasa ya mabadiliko, nami nikaondoka nao bila ya kusita,” alisema.
Alisema nia ya kuwachukua vijana hao ni kujenga chama kama taasisi ili kisonge mbele tofauti na ilivyo sasa na siyo kujenga jina la mtu kama watu wanavyotaka iwe au wanavyodhani.
Mbowe alisema akiwa na vijana hao pamoja na viongozi wengine, walifanya kazi kama timu ili kuhakikisha wanakiingiza chama hicho Ikulu, akiamini kuwa asingeliweza peke yake kukipeleka mbele chama hicho.
Aliwataja viongozi aliowachukua kutoka katika vyama vingine vya siasa kuwa ni pamoja na Mkurugezi wa Fedha wa chama hicho, Antony Komu, Tundu Lissu, Mabere Marando ambao walitoka NCCR – Mageuzi.
Wengine ni Godbless Lema, Saidi Arfi na Mchungaji Peter Msigwa ambao walikuwa TLP na Ezekia Wenje aliyetoka Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa mwenyekiti wa tawi moja la chama hicho huku Mwanza.
Alisema safari ya kukijenga chama sio lelemama kwani ni sawa na treni inayotoka Dar es Salaam kuelekekea Kigoma huku akiamini wote watafiki, lakini imekuwa tofauti kwani wapo walioshuka njiani.
“Safari yetu ya Kigoma toka Dar es Salaam ilikuwa ndefu sana … wapo walioshuka katika kituo cha kwanza tu Pugu, wengine Morogogo na vituo vingine vilivyofuata na kupata vilevile lakini tutafika tu,” alisema.
Akitoa historia fupi ya maisha yake katika siasa, Mbowe alisema aliingia akiwa kijana mdogo muasisi ambaye alipata nafasi ya kukiongoza chama kama mwenyekiti wa kwanza wa vijana, baadaye kupata nafasi mbalimbali ikiwamo uenyekiti.
Alisema aliingia katika chama hicho na kuchanguliwa kuwa kiongozi, lengo likiwa kufanya mabadiliko kwa vitendo na si kwenda kupata faida kama watu wengine wanavyofikiria.
“Lakini nilifanya kazi yangu ya kuijenga CHADEMA hatua kwa hatua kwa maana nyingine nimefanya kazi ya chama kwa miaka 23 sasa bila kulipwa mshahara wowote kwa sababu mimi ni mfanyabiashara,” alisema.
Alisema chama akitatoa maamuzi ya kumwonea mtu yeyote bali kitamhukumu mtu kutokana na makosa yake.
DEC12
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja-P3vpv8v160MGBn27SrtSkZ6D0_zjFplUItxeeNgvNO9UH9iXypnVH7tbvnYoGiYLe7eMyZuPe6qfVYaf33zKVC17lbjkdCC6yWQalwDoB9FdZkHhuISUtKjeAvIF4PvuzvWE1F22eYE/s640/NGI_3516.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzygHprAZw41eWGYacM9Eha8roKAqqHQS2SFD3n2G27y-GwJHJjgFQT8NjScTaZPeo3oqvVyKzCjSaxUTxdH8xc0fVFOm_Ba0JJ7rqvt6z5CDvE2QLEl4SuekKJQxooxHUglJY_db2kdLU/s640/NGI_3523.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhaSjprYLFZJznALzV5pX4fX2DnHHA7hdnh5LDb8UJBNlgltX3A_fmr6KxeOK-tNWD8JGCMwc5k9AU0CQHAw9Xj-y7HdwiwjDxyL2FnU5gZY8rJ1m4o_35l8wXeHmAjV3-AuZcLoNr4kHHM/s640/NGI_3524.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrk_MoiAMAM7IbIfrSSa2H0Cn43Wx35OLaaerIWKiqWP_mdjGUX_uQduvGN0wgzfSKNdreOOLuFrEpJc8l_tQnI993x8iWa6YHyom46wCvouIEUjY0Tyq5hN36kD1-CCzhBEfqEwHF5Psm/s640/NGI_3514(1).jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzsJLnztnDOh_inHBemFyvSh9xp0hzO6S0NlnifBkytedB3y03pR9OzZ3fxh28TV-D5Ar3VD-a7YWy9VzCFJFNsw1La0WWcW1Ne0tporCY0NhyruDK19_GPc-JpDMqHJpp9j5u10QaZ1Ld/s640/NGI_3513.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Barack Obama wa Marekani kwa viongozi mbalimbali wa Afrika wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiymS7uWiRX67K-l8FVHNAXf_2Ywm0uC_bJsDyAN2HyIfUcAdqOGJPLsJIJ02imeQSGVMJNCJcvXzQc3XSXKE899RF7aiWqGTbBovEDJP5c_fDLx7fDQxdnTK7EXfGwh2FfR2UpPO0Y6TGW/s640/NGI_3387.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013.Picha na IKULU
DEC12
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEicduapek9KHHIsXWOaTYSt9zU6OrSH26i8sqgJZuv99VXMio26j_7cQCpFRRHoUuRQ6jPWWiYdXOyJIy7t3iB98haBVQUonwqQZTTkR6TscxlzTrE9H5F1LpxfGCHAThxlsoSjqYv5k714/s1600/200px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png)
Serikali Mkoani Rukwa inapenda kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti la Jambo Leo toleo namba 1546 la tarehe 3, Disemba 2013 iliyoandikwa na Mwandishi Gurian Adolf katika ukurasa wa 10 iliyokuwa na kichwa cha habari "TCCIA Rukwa yaomba mbolea ya DAP".
Sehemu ya taarifa hiyo ilieleza kuwa; Nanukuu "Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Rukwa, Shadrack Malila ameiomba Serikali kuwashauri wakulima wa Mkoa huo kutumia mbolea nyingine ya kupandia mahindi badala ya mbolea ya minjingu ambayo haijafanyiwa utafiti katika Mkoa huo."
Kwa mujibu wa gazeti hilo taarifa hiyo aliitoa mbele ya waandishi wa habari Ofisini kwake mjini Sumbawanga ambapo aliongeza kuwa "Tangu awali wakulima hao walikataa mbolea hiyo, baada ya kuitumia kupandia na kushindwa kustawisha vizuri mazao yao ya mahindi, tofauti na mbolea ya DAP ambayo husaidia kupatikana kwa mazao mengi”. Mwisho wa kunukuu.
Serikali Mkoani Rukwa inapenda kukanusha kuwa sio kweli kwamba mbolea ya minjingu haijafanyiwa utafiti kufaa kutumika katika Mkoa huu na kwamba haijapokea malalamiko yeyote yaliyo rasmi kutoka kwa wananchi (wakulima) juu ya ubora na ufanisi wa mbolea hiyo. Matokeo yake yameonekana kuwa ni mazuri hususani baada ya mbolea hiyo kuboreshwa zaidi na sasa inaitwa "Minjingu Mazao".
Napenda ifahamike wazi kuwa tafiti mbalimbali za udongo zimefanyika Mkoani Rukwa mfano, taarifa ya BRALUP, 1977, Tafiti za udongo zilizofanywa na Kituo cha Utafiti cha Uyole na Sampuli mbalimbali zilizopelekwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kutoka Halmashauri ya wilaya ya Nkasi miaka ya 2008-2010 na kuonesha sehemu kubwa ya udongo wa maeneo ya Uwanda wa juu wa Ufipa (Ufipa Plateau) kuna upungufu mkubwa wa kirutubisho cha aina ya Naitrojeni kulingana na mahitaji yake kwa mimea jamii ya nafaka, hasa mahindi chotara.
Aidha, majaribio ya kutumia aina na viwango mbalimbali vya mbolea kwa zao la mahindi ikiwemo Minjingu yamefanywa kupitia Kituo Kidogo cha Utafiti cha Uyole kilichokuwa wataalam huko Nkundi na mashamba ya majaribio sehemu mbalimbali na kutoa matokeo yaliyofanyiwakazi. Kufuatia majaribio hayo, Mkoa wa Rukwa ulitoa mapendekezo kwa kampuni ya Minjingu Mines & Fertilizer ya kubadilishwa kwa umbile la mbolea ya Minjingu kutoka katika umbile la unga (powder form) na kuwa katika umbile la sasa la chengachenga ili kuwa rahisi wakati wa kuweka mbolea shambani. Pia Mkoa ulipendekeza mbolea hiyo iwekewe kirutubisho aina ya Nitrojeni ili kukidhi mahitaji ya udongo wa sehemu kubwa ya Ukanda wa juu wa Ufipa, mapendekezo ambayo yamezingatiwa zimefanywa na matokeo yake kuonekanika.
Mashamba Darasa yanayohusisha mbolea ya Minjingu Mazao yameanzishwa na kuendeshwa sehemu mbalimbali za Mkoa katika msimu uliopita wa 2012/2013 na kukaguliwa na Viongozi kuona ufanisi wake. Yapo mashamba yaliyofanya vizuri na yapo ambayo hayakufanya vizuri. Hali ya tofauti kama hiyo hutokea kwa aina zote za mbolea zinapotumika katika maeneo tofauti.Ikumbukwe kuwa ardhi ipo hai na hutofautiana kutoka sehemu moja na nyingine!
Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wakulima wengi wameshindwa kupata matokeo mazuri katika kilimo kwa kushindwa kufuata masharti ya wataalam wa kilimo hata kama wakitumia mbolea ya aina yeyote. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Profesa Kauzeni na wenzake katika vijiji vya Ntendo na Mtimbwa mwaka 1998, pamoja na mambo mengine ilibainika kuwa wakulima wachache waliomudu kutumia mbolea au mbegu bora hawakuzingatia viwango vilivyopendekezwa na wataalam. Walitumia karibu nusu tu ya mapendekezo, Mfano Hekta moja iliyopandwa mahindi zilitakiwa kutumia kilo 125 za TSP Triple Super Phosphate ( P2O5 ) 18% na kilo 250 za UREA (N)46%, ili kuvuna tani sita za mahindi sawa na kilo 6,000 au wastani wa magunia 60 kwa hekta. Waliofanya vizuri kidogo walitumia kilo 100 tu za TSP na kilo 100 za UREA.
Kufuatia taarifa hiyo, Uongozi wa Mkoa wa Rukwa haupendi kuingilia uhuru wa mtu wa kupata na kutoa habari kama Mtanzania mwingine yeyote. Ni vema mtu akatoa taarifa anazozifahamu vizuri/zilizofanyiwa utafiti, zisizoleta mtafaruku au kuipotosha jamii na zisizolenga kuvutia maslahi binafsi kwa namna yeyote ile.
Serikali ya Mkoa imesikitishwa na taarifa aliyoitoa Bwana Malila. Ni dhahiri kuwa ametumia vibaya nafasi yake ya uenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Rukwa kuwashawishi wakulima wa Mkoa huu kuwa mbolea ya Minjingu haifai na haitowapa mavuno mazuri. Ikumbukwe kuwa Bwana Malila ambae ni msambazaji wa pembejeo zenye ruzuku ya Serikali katika Manispaa ya Sumbawanga kwa mwaka huu 2013/14 pia ni mfanyabiashara wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea anayoipigia chapuo ya Diammonium Phosphate maarufu kama DAP.
Ifahamike pia kuwa Bwana Malila aliwahi kuwa na Mkataba na Kampuni ya Minjungu Mines & Fertilizer Ltd katika msimu wa kilimo wa mwaka 2009/2010. Kama kweli mbolea hiyo haifai mbona aliwahi kuwa wakala na akaisambaza kwa wakulima bila kutoa matamko kama haya? Ni dhahiri kuwa taarifa yake hiyo ina mgongano wa kimaslahi na hailengi katika kuboresha kilimo kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa.
Imetolewa na:
Albinus Mugonya,
Kaimu Katibu Tawala Mkoa,
RUKWA.
10 Disemba, 2013
DEC11
Bwana Ali Masoud au Maarufu kwa Jina la' Masoud Kipanya' na ambaye Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus, akizungumza na wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2013 Kingolwira Morogoro , pia kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka kufanya uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka, Akizungumza pamoja na wakazi wa eneo la Kingolwira pamoja na wageni mbalimbali waliotoka sehemu mbalimbali Tanzania na kutoa tamko rasmi la kuzindua shindano la Maisha Plus/ Mama shujaa wa chakula 2013
Mshindi wa Shindano la Maisha Plus Bernick Kimiro akizungumza na wageni wa alikwa pamoja na wenyeji wa eneo la Kingolwira Morogoro, kwa kuwasisitiza vijana wajitokeze kuchukua fomu za ushiriki katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2013 ambazo sasa zimesha anza kutolewa na kuwaeleza kuwa shindano hilo linatoa Fursa nyingi za kimaendeleo na kilimo kwa ujumla.
Bwana Bonda ambaye ni mmoja wa wakurugenzi Maisha Plus
Kulia ni aliyekuwa Mshindi Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sr. Matha Mwasu akiwa na Mshindi wa Tatu Bi. Tatu
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama shujaa wa Chakula 2013 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akifanya uzinduzi wa aina yake wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula 2012/13 kwa kufukua fomu ambazo zilikuwa zimefukiwa ikiwa ni kielelezo cha kilimo kwanza
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. AnthonyMtaka akizionesha fomu hizo baada ya uzinduzi huo.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka akimkabidhi Fomu ya kwanza ya ushiriki kwa Bi. Nuru Saidi Mbonga kutoka Dakawa ikiwa ni fomu ya Mama shujaa wa Chakula 2013
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka Akimkabidhi fomu ya Ushiriki wa Maisha plus kwa vijana Bi. Shamimu Ramadhani
Mmoja ya Vijana wakiume nae akiwa anakabidhiwa fomu ya ushiriki na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Anthony Mtaka
Wakiwa wanasoma fomu na kujiandaa kuzijaza
Burudani za Ngoma zikiendelea
Burudani za aina yake zikiendelea
Wazee kutoka eneo la Kingolwira wakiwa wamekuja kushuhudia uzinduzi huo
Wadau kutoka Sehemu mbalimbali wakiwa wamekuja shuhudia uzinduzi huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Ali Masoud 'Kipanya' akifunga sherehe fupi za uzinduzi wa Maisha Plus 2013
DEC11
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMjevu8H8i4QMkzXoqDPB1ome4ROBdnUx4Rolm75itQYN46xmTtEe2eMlR3WIUz3tZZVl8MEmq5p9_d9agU0B7LYyvp1jECzD8JrYbOXqsOaYZL-g8504_nUwMOEBPZ2JBkOKFmG3ZEyPR/s640/IMG_8388.jpg)
Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Badra Masoud akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kwamba shirika hilo kuwa hatarini kupelekwa mahakamani kufuatia kuvunja mkataba na kampuni ya McDonald Live Line Technology Limited iliyoshindwa kutekeleza zabuni iliyopewa kwa mujibu wa mkataba kati ya Pande hizo,kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo bw. Frank Mvungi.
----
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Limekanusha taarifa iliyotolewa na baadhi ya habari kuwa liko mbioni kufikishwa mahakama kutokana na kuvunja mkataba na kampuni ya McDonald Live Line Technology Limited.
Akikanusha taarifa hiyo Meneja Uhusiano wa shirika hilo Badra Masoud amesema kuwa shirika liliamua kuvunja mkataba na kampuni hiyo baada ya kushindwa kutekeleza zabuni waliyopewa ya kusafirisha, kusambaza na kuweka nguzo za umeme katika eneo la Kiyungi/Arusha 06 kV lines iliyotakiwa kukamilika ndani ya wiki 32 kuanzia Julai 28, 2010 na kuisha mwezi Machi 11, 2011.
Badra aliongeza kuwa baada ya mkataba huo kuvunjwa kampuni ya McDonald ilifungua shauri katika Tume ya Usuluhishi na Ushindani ambapo mara baada ya pande zote kusikilizwa kampuni hiyo iliamriwa kuilipa TANESCO fidia ya zaidi ya milioni 700.
DEC11
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEim42kUQORcXp9XFzrtCJriEhKrc0vQBsA_ShH4l9VBHFjpVP8qlUzurXQDJelavXOAlbMTCXUHFgU8z6DAGoG3_APyctnzYQqhZUeHrgQhNDdKarynFY6Z5_Cz6_-E7i5alBOQuRzv4R1g/s1600/8-chadema.jpg)
December 7 / 2013.
Chadema Students’ Organization (CHASO) ni umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo iliyo chini ya Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) taifa iliyoanzishwa chini ya kanuni ya Mabaraza ya chama katika kipengele 7.8.2(a) cha katiba ya chadema
Msimamo:
Umoja wa wanafunzi wa vyuo (vikuu) wanachadema / Chadema Students Organisation(CHASO)IRINGA, unatamka rasmi wazi kwamba tunaunga mkono kwa asilimia zote maamuzi yaliyotolewa na kamati kuu ya chama Makao makuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuhusiana na kuvuliwa nyadhifa za uongozi kwa baadhi ya viongozi ndani ya chama.
Tukiwa ni taasisi ya Chama inayoundwa na wanafunzi wa elimu ya juu Mkoani Iringa, tunakubaliana moja kwa moja na maamuzi ya chama, pia tunaungana na wenzetu wa CHASO Kanda ya Dar-es-salaam kulaani vikali vikundi vya kihuni vinavyotumia vibaya jina la CHASO kutoa matamko yanayopingana na maamuzi ya kamati kuu ya chama; kwani kama weledi ni wazi kwamba wanaelewa taratibu kamili zinazopasika kufikia hatima mahususi.
Maamuzi ya kamati kuu ya chama yanaonesha wazi na dhahiri kwamba Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ni chama kipevu yaani kilichokomaa na chenye misimamo yake: kisichoogopa Umaarfu wa Mtu bali ni chama kinachosimamia na kufuata misingi ya kikanuni na taratibu (katiba) iliyojiwekea.
Tunawaomba Watanzania kutoamini katika ushabiki wa kisiasa unaoendelea ama kutokuwa washabiki wa umaarufu wa mtu fulani ama kikundi fulani cha watu, katika kufikia maamuzi juu ya suala lolote katika jamii; pia tuwe wafuatiliaji na waelewa kwa kina juu ya mambo yanayohusika ili tuweze kufikia maamuzi sahihi bila upotofu (kupotoshwa).
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesimamia dhana ya uwajibikaji katika ngazi zote bila kuangalia ama kuogopa nyadhifa au nafasi ya mtu, bali kuhakikisha utaratibu unafuatwa katika kufikia maamuzi bila woga, pasipo kuathiri matakwa ya kikatiba.
Watanzania wote kwa ujumla: wasomi kama dira ya jamii huu ni wakati ambao tunatakiwa kutumia uledi na busara katika kuangalia mambo(uchambuzi) kwa upeo mpevu. Ni rai kwetu kwamba si vema kutoa shutuma dhidi ya chama bila kufuatilia ama kuelewa taratibu na kanuni (katiba) zinazopasika katika kufikia maamuzi sahihi. Maamuzi sahihi sio lazima yamfurahishe kila mtu bali kulinda maslahi ya Chama na Umma kwa ujumla wake.
Watanzania hatupaswi kukurupuka kiushabiki na hurka binafsi/mihemko ama jazba na gadhabu kwani kwa kufanya hivyo tutawapa nafasi watu wenye hinda katika gurudumu la mabadiliko tunayoyaelekea hivyo tunapaswa kuwa makini.
Kimsingi tunatakiwa kuwa watu wenye Mantiki na upembuzi yakinifu katika kufikia maamuzi kwa kuzingatia uhalisia wa dhana ya uwajibikaji; hivyo basi, katika kuyaelewa mambo na tufanye tafiti za kina ili kuweza kufikia maamuzi ya kuamini watu wengine katika usahihi wake, hivyo kutozipa nafasi hisia za propaganda za mamluki.
Tunawaomba Watanzania wote katika makundi mbalimbali, kuondokana na dhana ya ushabiki katika mambo ya msingi kwani mpango wa Chadema ni kuangalia na kulinda maslahi ya Umma na siyo kujenga jina ama umaarufu wa mtu mmoja mmoja, pia chama siyo sehemu ya malumbano; hivyo shauku yetu ni kujenga wanachama Imara na siyo kupata mashabiki kabambe. Chadema itaendelea kuwa chemchemi ya Ukombozi wa Taifa na ujenzi wa viongozi wenye nidhamu, haki na uwajibikaji.
Pia tutumie fursa hii kuwaonya watu wanaotumiwa kusambaza propaganda zenye lengo la kuendeleza marumbano yasiyo na msingi.
Mwitikio wa vyama vya siasa nchini umekuwa ni watofauti kwa kuwa vinara wa kuleta mkanganyiko baina ya watanzania na uvumi wa propaganda; swali rahisi la kujiuliza wana maslahi gani juu ya maamuzi ya CHADEMA ama mtu yeyote ndani ya CHADEMA?, pia tunawataka watanzania waelewe kwamba malengo ya timu (wachezaji katika timu ni kuhakikisha wanafunga goli ili kupata ushindi mchezaji anayepiga chenga nyingi na kukimbia na mpira mpaka nje ya uwanja anakuwa hafai anapaswa kukaa benchi).
Tunawaomba watanzania tushikamane katika kipindi hiki cha mpito, tukielewa ya kwamba tunapaswa kuwa makini na propaganda zinazofanywa na makundi ya watu wenye lengo baya la kurudisha nguvu ya harakati dhidi ya mabadiliko tunayoyakusudia, kwani kila mapinduzi au mageuzi yanakwenda na usaliti. Chadema kitaenzi mawazo na mchango mzuri wa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na chama kwa maslahi ya Umma.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA.
TIMOTHEO J. MKANYIA..............MWENYEKITIKITI CHASO IRINGA 0713739683
ANDEMBWISYE ISRAEL…………………….KATIBU CHASO IRINGA 0764969838
MICHAEL NOEL…………………KATIBU MWENEZI CHASO IRINGA 0716746442
MWENYEKITI CHASO
DEC11
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4l7iWMSexlvJ6EZkqtYXviSmRIuLignhicXpMnUG34_o12CfBcqBbrxbqpL4NMW_bK6LTBWY2XBILbVXd9T4WXdcBEYQHdj4RfUzKlOVCo9Me8oa0hR0P7KesEqDa-KTS2Ydzkwgm6SA5/s640/09.jpg)
Maandamano yakipita mbele ya Jukwaa Kuu na mabango ikiwa ni sehemu ya ufunguzi Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,jana.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8iocaiCMflJW0XYY7WRAESc-qq_uQ2sS9ikKpuHwA2couUzburZiAI1Mx3YvTMVo-2w-g9Mgikx3jGLzei3KYIzr9km7mbMHuaPocSCp534Ky7kvTB78V2umoroGBx8mqsJff45rTmxqS/s640/02-1.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akikata utepe kuashiria kuzindua Kitabu cha Mpangokazi wa Taifa wa haki za Binadamu wa mwaka 2013-2017, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,jana . Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Naibu wake, Angela Kairuki (kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Hakiza Binadamu na Utawala Bora, (wa pili kulia.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjLdCgq_wXq8Mt7m035n3EKAzk2jElhZJm56OAMiqpUhZP1DoDLXyioUoI2x_F6TfL4hsl0GJU2KCuaaLGb0vjUS4CeSG3XnqNk6QjVBcnQmzOKya1bWxOINg1FcCBIrBzxNzftJRMyu1aL/s640/01-11.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Kitabu cha Mpango Mkakati wa Haki za Watoto 2013-2017, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,jana . Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCN59csFdpj9KQvNLQRuKDo0ry7GkogmEKdONEQwzSiCTAb3aMK-YCpqk6GnUES0M3qJ1mDC1_wo_6u5hp8tlKQktMMs6SUdcsWz4wBj8HMbKVvuER61QrIDAXKiP0vRie0aLPVAK9Sgh-/s640/1112.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mrakibu Mwandamizi wa Mwandamizi wa Magereza, Isaack Kangura, wakati alipotembelea Banda la maonyesho la Magereza katika Viawanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili,jana .
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6H1OYM-Ui0wou4oe-gUxDM5LlyNBeTmSSeLMvFP3pssZRsK6oyK4iBzY0vlRLZ9teVm_KikFiTiAKWo_c22DTWZS4RfrMUyu-ev5f57SZuyDEuTByj8QlxVFaiOGAyYW_VDIBE2jdONsU/s640/03-1.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSncNukY6HO7Fd3Zb7ERIrabtebLJBB2B4r83Af24GulcgV5ZwOGqzNYRmu6JkgQ84674HH9DcofjIBS9sPtAZYHPSIzU1ZpF1h6s2Q0t7k7mny3jDQjv7HENLTpIr_UXK0PNV2eGYPwtr/s640/061.jpg)
Baadhi ya wafanyakazi wa Mashiriki, Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana .Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
----
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnXUSIKY65Z1WGyYOKozETvsuQwDvLfNnkVwiar6ZObBx62_Tg8k-rfjs7YR0zkyaKofitvm0tMaKP1iL66UG8HW_wdPOAnB4SNAz29GY_56eH6l714PCjlWCHIs41r5SoWXvAb9dpTRwK/s1600/200px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png)
HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA SITA YA KITAIFA YA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU NA MAADILI, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM,TAREHE 10 DESEMBA 2013.
--
Mheshimiwa Mathias Chikawe, Waziri wa Katiba na Sheria;
Mheshimwa Angela Kairuki, Naibu Waziri Katiba na Sheria;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi;
Mheshimiwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Kiongozi mstaafu Ameir Manento;
Mheshimiwa Jaji Kiongozi, Faki Jundu;
Mheshimiwa Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa hapa Tanzania, Joyce Mends- Cole;
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
Waheshimiwa Makamishna wa Tume na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria;
Waheshimiwa Mabalozi;
Waheshimiwa Viongozi mbalimbali wa Serikali; Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi;
Viongozi wa Vyama vya Siasa, Dini na Jumuiya za Kijamii;
Wageni Waalikwa;
Ndugu Wanahabari;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana.
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kukusanyika hapa leo, kushuhudia Maadhimisho haya ya Siku ya Haki za Binadamu na Maadili ambayo husherehekewa Duniani kote Desemba 10 kila mwaka.
Nitumie nafasi hii pia kuwakaribisha na kuwapongeza nyote mliofika mahali hapa. Mmefanya hivi kutokana na sababu moja tu kubwa, nayo ni kwamba; Kila mmoja wenu anatambua na kujali umuhimu wa Haki za Binadamu na Maadili mema ndani ya jamii yetu.
Niwashukuru pia wale wote waliofanikisha tukio hili kwa njia moja ama nyingine. Kipekee niwashukuru Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Wizara ya Katiba na Sheria, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Umoja wa Mataifa -Tanzania, kwa jitihada zao kubwa za kuratibu na hatimaye kufanikisha Maadhimisho haya. Hongereni sana.
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana;
Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku hii kutokana na ukweli kuwa sisi ni wanachama wa Umoja wa Mataifa ambako ndiko chimbuko la Haki za Binadamu, na kwamba kama Taifa, tunawajibika moja kwa moja kuzikuza, kuzilinda na kuzitekeleza hapa nchini.
Serikali ya Tanzania inao wajibu wa kulinda na kukuza Haki za Binadamu kama ilivyoelezwa na kufafanuliwa ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Mikataba ya Kimataifa na Kikanda ya Haki za Binadamu na sheria mbalimbali za nchi.
Kwa kutimiza wajibu wa kulinda na kukuza Haki za Binadamu, Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilizoridhia mikataba mingi ya kimataifa inayohusu Haki za Binadamu. Baadhi ya mikataba hiyo ni pamoja na; Tamko la Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu la 1948; Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa 1966; Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni 1966; Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto 1989; Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa aina zote za Ubaguzi wa mwaka 1965; Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa Ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya Wanawake wa mwaka 1979; Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu wa mwaka 2008; Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Haki za Watu wa mwaka 1981 na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Watoto wa mwaka 1990.
Baadhi ya mikataba hii tayari imeingizwa katika sheria zetu za nchi, ama kwa kuunda sheria mpya au kurekebisha zile zilizopo, ili kuhakikisha kuwa ulinzi wa Haki za Binadamu unaimarishwa.
Aidha, pamoja na kuridhia mikataba hii, Serikali imekuwa ikiandaa ripoti mbalimbali za utekelezaji wa Haki za Binadamu ambazo zimekuwa zikiwasilishwa kwenye vyombo vya kimataifa kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa mapendekezo ya utekelezaji.
Ndugu Wananchi;
Napenda niwahakikishieni kuwa Serikali inaendelea kupitia mikataba ambayo bado haijafanywa kuwa sehemu ya sheria za nchi, ili nayo iweze kuingizwa kwa kadri inavyofaa kwa maslahi ya wananchi wetu na maendeleo ya nchi yetu.
Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kinara wa kujali Haki za Binadamu, Serikali imeanzisha taasisi mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya kulinda na kukuza haki nchini. Taasisi hizo ni pamoja na:- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi; Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); Bunge na Mahakama. Vyombo hivi vilianzishwa kwa mujibu wa sheria na tutazidi kuvipa ushirikiano kadri inavyowezekana ili viendelee kufanya kazi zake vizuri na kukidhi matarajio yake kwa umma.
Serikali pia imejenga mazingira mazuri na kuruhusu taasisi zisizo za kiserikali kuanzishwa kwa lengo la kusaidia juhudi zake za kuimarisha Haki za Binadamu hapa nchini. Hadi sasa, Tanzania ina takribani mashirika 5,000 yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na utetezi wa Haki za Binadamu. Mashirika haya yanatambuliwa kwa mujibu wa mikataba mbalimbali ya kimataifa na sheria za nchi. Baadhi ya mashirika hayo ni pamoja na; LHRC, NOLA, PINGOs, TPCF, TAWLA, ZLSC, WLAC, SIKIKA, SAHRINGON, TGNP, HAKIELIMU na HAKI-ARDHI. Mashirika haya yamekuwa yakitoa mchango mkubwa katika kutetea na kulinda Haki za Binadamu hapa nchini.
Serikali pia imetengeneza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ambao utazinduliwa leo kwa lengo la kuhakikisha kila sekta inajumuisha masuala ya Haki za Binadamu kwenye mipango kazi yake na utekelezaji wake.
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana;
Eneo lingine muhimu ambalo Serikali inajivunia katika harakati zake za kujenga misingi imara ya Haki za Binadamu hapa nchini, ni haki ya kupata elimu ambapo hadi sasa, zaidi ya asilimia 98 ya watoto wenye umri wa kwenda shule, wanaandikishwa na kupata elimu ya msingi inayotolewa bure. Hivi sasa kila kata nchini ina shule ya msingi na sekondari, kata zingine zina shule zaidi ya moja. Haya ni mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Haki za msingi za Binadamu.
Ndugu Wananchi;
Maadhimisho haya yanatoa fursa nzuri kwetu sote kujiuliza; tumefanya nini katika kipindi cha mwaka mzima na changamoto zinazokabili suala zima la Haki za Binadamu. Tukumbuke kuwa utekelezaji wa Haki za Binadamu na Maadili ni mchakato, hivyo siku zote ni lazima tuendelee kuboresha haki hizo, kama vile ambavyo haki hizo pia huibuka na kuongezeka kila mara.
Napenda pia kuwahakikishieni kwamba Serikali yenu inajitahidi kuhakikisha kuwa wananchi wote hasa wale wa kawaida, wanapata msaada wa kisheria kwa kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo:- Kuanzisha mchakato wa kuwa na Sekretarieti ya Huduma za Kisheria; Kuboresha Mahakama za Mwanzo; Kuanzisha Shule ya Taaluma ya Sheria na Kuongeza idadi ya majaji wa Mahakama za Rufaa kutoka wanane mwaka 2005 hadi kufikia 14 mwaka 2012 , na wale wa Mahakama Kuu, kutoka 24 hadi 54.
Ndugu Wananchi;
Pamoja na juhudi kubwa za Serikali kuboresha mazingira ya upatikanaji na utoaji wa Haki za Binadamu nchini, matukio ya ukiukaji wa haki hizo yameendelea kuongezeka. Taarifa za vyombo mbalimbali vya habari na ripoti za kitafiti, zimeonesha na kuthibitisha uwepo wa matukio kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini. Baadhi ya matukio hayo ni kama yale ya Ghasia zinazohusiana na vurugu za makundi; Mahabusu kuwekwa rumande muda mrefu kabla ya kesi kusikilizwa; Unyanyasaji dhidi ya wanawake na watu wenye ulemavu wa ngozi; Unyanyasaji wa watoto (ikiwemo ukeketaji, ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, mauaji kwa wanaozaliwa na ulemavu, utekaji nyara, ajira mbaya nk.) Nawahakikishieni kwamba Serikali imejipanga vema kukabiliana na kutokomeza uovu huo pasi kumwonea huruma mtu yeyote anayejihusisha na maovu hayo.
Tukumbuke kuwa watoto wanachukua nusu ya idadi ya Watanzania wote. Tunajua kwamba mafanikio katika utekelezaji wa haki mbalimbali za mtoto, ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya nchi yetu hususan katika kufanikisha Malengo ya Milenia. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha kwamba haki ya mtoto inalindwa sio tu kutokana na kwamba tunaiwakilisha Serikali bali kama wazazi, majirani na jamii kwa ujumla.
Leo hii pia, tunajivunia kuzindua Mkakati wa Miaka Mitano wa Kuendeleza Mageuzi ya Haki ya Mtoto 2013-2017. Tunazindua mkakati huu sambamba na Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Haki za Binadamu kuonesha dhamira ya dhati ya Serikali kulinda, kuendeleza na kuhamasisha haki za watoto .
Mkakati huu wa Haki ya Mtoto unaainisha hatua zinazopaswa kuchukuliwa na mawizara idara, mawakala na CSOs kwa miaka mitano kuhakikisha watoto wote ambao haki zao zimekiukwa, wanapata haki na kwamba mtoto yeyote anayekwenda mbele ya vyombo vya sheria, aidha awe muhanga, shahidi au aliyeonewa, anapata haki halali inayozingatia hadhi na utu wake kwa wakati.
Ndugu Wananchi;
Nitumie fursa hii pia kuwaasa Watanzania wenzangu kuanzisha kampeni maalum za kukuza maadili katika ngazi mbalimbali zikiwemo zile za utumishi wa umma, taasisi za dini, taasisi za elimu na katika nyanja zote za maisha ya kila siku. Suala hili likifanyika vizuri, naamini sote kwa pamoja, tutakuwa tumetimiza wajibu wetu wa malezi bora kwa watoto na vijana wetu hali itakayosaidia kupunguza maovu mengi ndani ya jamii.
Ndugu Wananchi;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kabla sijahitimisha hotuba yangu, napenda kusisitiza kuwa usimamizi wa Haki za Binadamu na ujenzi wa Maadili mema ndani ya jamii yetu, ni jukumu la kila mmoja wetu. Kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine anawajibu wa kulinda, kuheshimu na kudumisha Haki za Binadamu. Nawahakikishieni kwamba Serikali ya Awamu ya Nne inatilia maanani sana suala la Haki za Binadamu, Utawala Bora na Maadili. Tukishikamana katika hili naamini tutashinda kwani “ Umoja ni nguvu”
Nawaasa kujiepusha na mambo yote yanayochangia kwa njia moja ama nyingine, kuvunja na kukiuka misingi ya Haki za Binadamu na Maadili mema. Kueni raia wema na chukieni maovu.
Baada ya kusema hayo, kwa heshima na taadhima natamka kuwa; Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu na Maadili, yamefunguliwa rasmi.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza
DEC11
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmU1jBnqFjz_ACgA7CsT9-jkYAKgmp4KqupfV5c1SAxXeuLc1FCywnFPOgNZAnkVkEt2_SqNBL8PWwgp4S2M2whtCj9Hjl4SohJCboyWkC3IzA3Jz2JeLgOy9wuxJ0fKJ8N9BuMIfe7bxA/s640/2.jpg)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akitoa maelezo juu ya maendeleo ya sekta ya nishati kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ubou Sabaa (aliyeketi upande wa kulia). Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya sekta ya nishati katika maeneo ya ulipaji kodi, mapato, ujenzi wa bomba la gesi ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa shirika la Tanesco.
0 comments: