Mkapa aiponda misaada kutoka nje - asema yadhoofisha uchumi Afrika
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Benjamin William Mkapa amesema misaada inayotolewa na nchi za
Magharibi kwa nchi za Afrika haina masilahi na ina lengo la kudhoofisha
ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika .
Alisema
kuwa mara nyingi nchi za Magharibi zimekuwa zikitoa misaada kwa
masharti ya kutolewa kwa ushuru kwa bidhaa zinazoingia pamoja na bidhaa
zinazouzwa katika mataifa hayo, jambo ambalo linaweza kudhoofisha ukuaji
wa uchumi kwa nchi za Afrika .
Kauli
hiyo aliitoa wakati akifungua Chuo cha Ualimu cha Benjamin Mkapa
kilichopo Mchangamdogo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni
katika shamra shamra za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Alisema
masharti hayo yanapaswa kuepukwa na viongozi wa nchi za Afrika na
kusisitiza kwamba hayo yanaweza kuepukika ikiwa mataifa hayo yatawekeza
zaidi katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha wanawaandaa vijana kwa
kuwapatia elimu bora .
“Misaada
hii ina lengo la kudhoofisha ukuaji wa uchumi kwa mataifa ya Afrika,
hivyo ni vyema viongozi wa mataifa hayo kuwa makini na masharti
yanayotolewa , unafikiri unapoambiwa bidhaa zinazoingia nchini mwako
zisitozwe ushuru Serikali itapata wapi mapato ? ” alihoji .
Akizungumiza
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar , alisema kuwa yameleta faida nyingi
kwa Wazanzibari hasa katika sekta ya elimu ambapo yameondoa ubaguzi
katika upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii ikiwamo elimu, afya na
mawasiliano.
Alibainisha
kwamba kufanyika kwa Mapinduzi hapo Januari 1964 kuliondoa aina zote za
udhalimu wa kikoloni ambao uliwafanya wenyeji wa visiwa hivi kuwa nyuma
kutokana na kukosa fursa ya
“Ni
lazima tukiri kwamba Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ndiyo yaliyowaweka
wananchi wa Zanzibar katika hali ya umoja , kupendana na kusaidiana
kwani yaliondoa minyororo ambayo ilikuwa inakwaza kufikia maendeleo
”alieleza Mkapa.
0 comments: