Jengo la makao makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa ufipa Kinondoni yameviwa ma vijana waendesha boda boda wa jijini Dar muda huu wakitaka waonane na viongozi wa chama hicho kuwaeleza kero na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa maofisa wa jiji pamoja na askari polisi katika utekelezaji wa mujukumu yao ya kujipatia riziki. Kutokana na hali hiyo tayari polisi wameshazingira eneo zima la makao makuu ya CHADEMA kwa ajili ya tahadhari ya jambo lolote.

0 comments
Jengo la makao makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa ufipa Kinondoni yameviwa ma vijana waendesha boda boda wa jijini Dar muda huu wakitaka waonane na viongozi wa chama hicho kuwaeleza kero na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa maofisa wa jiji pamoja na askari polisi katika utekelezaji wa mujukumu yao ya kujipatia riziki.

Kutokana na hali hiyo tayari polisi wameshazingira eneo zima la makao makuu ya CHADEMA kwa ajili ya tahadhari ya jambo lolote.









Read More »

Ajali mbaya mlima Sekenke - Lori la Mafuta lateketeza wanne kwa moto

0 comments



Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua

Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii

Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii



Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa


Hii ni njia ya mlima sekenke

Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwam kwenye Lori hiloo

Moto ukimalizikia kwa mbaliii kama inavyoonekana

Read More »

TANGAZO LA AJIRA 517 SERIKALINI

0 comments


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/E/34
17 Februari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).Pamoja na kazi zingine chombo hiki
kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa
Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 517 za kazi kwa waajiri mbalimbali
kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu
tawala Mkoa Pwani, Katibu tawala Mkoa Simiyu, Katibu tawala Mkoa Katavi, Katibu
tawala Mkoa Iringa, Katibu tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu
tawala Mkoa Kagera, Katibu tawala Mkoa Rukwa na Katibu tawala Mkoa Njombe.
Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri
ya wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Nafasi hizi pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Muleba,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri
ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi
Halmashauri Manispaa Arusha, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma,
Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa
Tabora.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa kwa sharti hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa
batili.
v. Waombaji wanatakiwa kuambatisha maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V)
yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Machi, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiv.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
xvi. Pamoja na waombaji kuainisha waajiri, Sekretarieti ya Ajira baada ya usaili
itawapangia waombaji waliofaulu, kwa mwajiri yoyote bila kujali chaguo la
mwombaji.Hii ni kutokana na baadhi ya waombaji kupendelea kufanya kazi
kwenye baadhi ya maeneo tu.
Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika
Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,
Secretariat,
SLP.63100,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
1.0
AFISA LISHE II (NUTRITION OFFICER II) – NAFASI 21
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kukusanya taarifa na takwimu za lishe kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali
na kutoa ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi ya wilaya.
 Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa ya watoto na makundi mengine
yenye lishe duni.
 Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya lishe katika ngazi ya wilaya.
 Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya lishe katika ngazi ya wilaya.
 Kusimamia kazi za lishe katika wilaya
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajriwa wenye Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi
na Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and
Nutrition, Food Science and Technology and Food Science) au Stashahada ya juu
ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
2.0
MSAIDIZI LISHE (NUTRITION ASSISTANT) – NAFASI 16
2.1 KAZI NA MAJUKUMU
 Kutambua na kuorodhesha na kuweka kumbukumbu za watoto chini ya miaka
mitano na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni ngazi ya kijiji na kata.
 Kufuatilia na kutoa ushauri wa lishe kwa kaya zenye watoto wenye lishe duni.
 Kuelekeza watoto na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni wapelekwe
kwenye kituo cha afya Kwa huduma zaidi.
 Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za lishe zinazotolewa kwa
makundi mbalimbali kwenye kata/kijiji.
 Kukusanya taarifa na takwimu za lishe katika sehemu yake ya kazi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye cheti cha miaka miwili cha
mafunzo ya lishe kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS A kwa mwezi
3.0
MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT)– NAFASI 12
3.1 KAZI NA MAJUKUMU
 Kulea watoto katika vituo vya malezi ya awali ya watoto wadogo mchana.
 Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi bora ya awali ya watoto wadogo
wenye umri wa miaka 0-8.
 Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya watoto vijijini/sehemu au eneo la vituo.
 Kuwa kiongozi wa kituo cha malezi ya awali ya watoto wadogo.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu mafunzo ya mwaka mmoja ya
malezi ya awali ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0-8 kutoka katika
Chuo kinachotambulika na serikali au wenye cheti cha mwaka mmoja cha mafunzo
ya ustawi wa jamii.
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B Kwa mwezi
4.0
AFISA USTAWI WA JAMII II (SOCIAL WELFARE OFFICER II)– NAFASI 184
4.1 KAZI NA MAJUKUMU
 Kuendesha usaili kwa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye
matatizo, pamoja na watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali).
 Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao
kamili.
 Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa.
 Kupokea na kukusanya taarifa za ustawi wa jamii kutoka kwa wadau na vituo
mbalimbali vya ustawi wa jamii.
 Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu,
wazee malezi ya watoto na familia zenye matatizo.
 Kupokea kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji wa vituo vya
kulelea watoto wadogo mchana, malezi ambao (foster care) na vyuo vya malezi
vya watoto wadogo mchana.
 Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka
kwa akina mama waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja.
 Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au
wanaohitaji misaada mbalimbali.
 Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye
familia na watu wenye dhiki.
 Kuhoji na kuandaa taarifa za washtakiwa.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya B.A (social work or sociology) au stashada ya juu ya
Ustawi wa jamii (Advanced Diploma in Sociol work) kutoka chuo cha juu
kinachotambuliwa na ustawii wa jamii.
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
5.0
MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE ASSISTANT
II) – NAFASI 24
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na mazingira
hatarishi.
 Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum na mazingira
hatarishi.
 Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na
watu wenye dhiki.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya mwaka
mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi.
6.0
MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II (KITCHEN/MESS ATTENDANT)
– NAFASI 4
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusafisha Vyombo vya kupikia.
 Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.
 Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.
 Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani.
 Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.
 Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne.
6.3 MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
7.0
AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II) – NAFASI 6
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
 Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili
isiyozidi hekta 10,000.
 Kufanya utafiti wa misitu.
 Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.
 Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
 Kukusanya takwimu za misitu.
 Kufanya ukaguzi wa misitu.
 Kupanga na kupima madaraja ya mbao.
 Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.
 Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu
ya miti kwa wananchi.
 Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
 Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au
Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
8.0
MSAIDIZI MISITU DARAJA LA II (FORESTRY ASSISTANT GRADE II) –
NAFASI 75
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kukusanya mbegu
 Kuhudumia na kutunza bustani za miti.
 Kutunza na kuhudumia miti na misitu.
 Kufanya doria.
 Kusimamia ukusanyaji mbegu na bustani za miti.
 Kukusanya takwimu za misitu.
 Kusimamia kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu.
 Kukusanya maduhuli.
 Kupima mazao ya misitu.
 Kufanya doria.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au
Stashahada (Diploma) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B/C kwa mwezi.
9.0
MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURE GENERAL) – NAFASI 10
9.1 KAZI NA MAJUKUMU
 Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa
upande wa nadharia na vitendo.
 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa
Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa
kazi.
9.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agriculture
General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia
(Teaching Methodology)
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
10.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRONOMY) – NAFASI 4
10.1 KAZI NA MAJUKUMU
 Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa
upande wa nadharia na vitendo.
 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa
Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa
kazi.
10.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agronomy)
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
11.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HORTICULTURE) – NAFASI 1
11.1 KAZI NA MAJUKUMU
 Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa
upande wa nadharia na vitendo.
 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa
Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa
kazi.
11.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Horticulture) kutoka
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
12.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HUMAN NUTRITION) – NAFASI 1
12.1 KAZI NA MAJUKUMU
 Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa
upande wa nadharia na vitendo.
 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa
Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa
kazi.
12.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Human Nutrition)
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
13.0 AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 71
(LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27
NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO
YANACHAMBULIWA.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
 Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
 Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
 Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
 Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
 Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
 Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,
 Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,
 Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
 Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao
mengine,
 Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,
 Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
 Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
 Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla
ya kupitishwa,
 Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
 Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
 Kufanya utafiti mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo
cha umwagiliaji,
 Kufanya utafiti wa udongo,
 Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,
 Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,
 Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi
maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya
sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
13.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa
mwezi.
14.0 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 38
(LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27
NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO
YANACHAMBULIWA.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
 Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
 Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,
 Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
 Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu
za umwagiliaji,
 Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
 Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji
pamoja na matumizi ya maji,
 Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
 Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na
wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
 Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na
 Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji
ipasavyo.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka
Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
14.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa
mwezi.
15.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 2 (LINARUDIWA)
KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013
WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusaidia kuunda boti za uvuvi
 Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
 Kufanya matengenezo ya boti.
 Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
 Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.
15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye stashahadaya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
15.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
16.0 DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II (FERRY / BOAT OPERATOR) – NAFASI
1 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27
NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO
YANACHAMBULIWA.
MAJUKUMU YA KAZI
 Kufunga na kufungua kamba za kivuko.
 Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.
 Kupanga abiria au magari kwenye kivuko.
 Kuendesha na kuongoza kivuko.
 Kutunza daftari za safari ya kivuko.
 Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
 Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
16.1 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na
kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine
Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda
usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha
majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.
16.2 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa
mwezi.
17.0 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II) – NAFASI 8
(LINARUDIWA). KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27
NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO
YANACHAMBULIWA.
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.
 Ataratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
 Atasaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
 Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo
kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
 Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani kwake
na mkoani.
 Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
 Atafanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya
mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
 Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama
katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
 Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
 Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
 Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa
malisho.
 Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
 Atafuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
 Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na
mkuu wake wa kazi.
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya
Mifugo(Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa
inayolingana nayo.
17.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
18.0 MHASIBU MSAIDIZI (ASSISTANT ACCOUNTANT) - NAFASI 3
18.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kupokea na kulipa fedha.
 Kutunza daftari ya fedha.
 Kufanya usuluhisho wa hesabu za benki
 Kukagua hati za malipo.
 Kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha.
 Kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu.
18.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti cha kufaulu mtihani mgumu wa Uhasibu Serikalini (Higher
Standard Government Accountancy Examination) unaotolewa na Tume ya
Utumishi wa Umma. Au
 Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyyote
inayotambuliwa na serikali.
18.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi
19.0 AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
19.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja (
Jointy Venture )
 Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
 Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
 Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
 Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishi katika vyama vya ushirika vya
Msingi.
19.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma)
katika fani ya Ushirika (Cooperative management and accounting) kutoka vyuo
vinavyotambulika na Serikali.
19.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
20.0 AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
20.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa makisio ya vifaa vinavyohitajika
(Material Requirement Budget) na Mpango wa Ununuzi (Procurement Plan).
 Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji za Wazabuni mbalimbali.
 Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji, na usambazaji wa vifaa.
 Kusimamia utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
 Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical Distribution).
 Mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design).
 Kusimamia ukaguzi wa kuhesabu vifaa mara kwa mara (Perpetual Stock
Checking) ghalani.
 Kutayarisha Taarifa za kazi katika vipindi maalumu.
 Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kila mwisho wa
mwaka (Annual Stock Taking).
 Kufanya kazi zingine ambazo atapangiwa.
20.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara (B.Comm) yenye mchepuo wa ugavi au
Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advanced Diploma in Materials Management)
inayotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya usimamizi wa Vifaa.
20.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D mwezi.
21.0 AFISA UGAVI MSAIDIZI II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER) – NAFASI 1
21.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.
 Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa
ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.
 Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.
 Kufungua “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa
na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
 Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.
 Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na
kwa usalama.
 Kuandaa hati za kupokelea vifaa.
 Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
21.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye cheti cha “National Store-Keeping Certificate au “Foundation
Certificate” kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti
kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
AU
 Kuajiriwa wenye Diploma ya Kawaida “Ordinary Diploma in Materials
Management” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa
Vifaa.
21.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.A na B kwa mwezi.
22.0 AFISA UTAMADUNI II (CULTURAL OFFICER GRRADE II) – NAFASI 1
22.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kutafiti masuala ya Lugha, Sanaa, Mila na Desturi katika ngazi ya Wilaya.
 Kufundisha fani mbalimbali za utamaduni katika Vyuo na Vituo vya Elimu na
mafunzo ya utamaduni.
 Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.
22.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada au stashahada ya juu katika Sanaa, Lugha au Sayansi ya
Jamii na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.
22.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
23.0 AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT
OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
23.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kuratibu na kisimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana
 Kuratibu shughuli za mikopo/mifuko ya Vijana
 Kuhamasisha vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini
 Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na
Afya ya Vijana
 Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, Ajira kwa Vijana na Elimu ya Familia kwa
kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali (NGO)
 Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu Vijana
 Kuratibu shughuli mbalimbali za NGO zinazoshughulikia masuala ya Vijana
 Kuandaa mipango ya kuboresha malezi ya Vijana
 Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo
nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali
 Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo Vijana ili kuwawezesha
kujiajiri
 Kuandaa mipango ya kuwahamasisha Vijana ili kuanzisha miradi midogomidogo
ya kujiajiri.
23.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (BA. in Sociology or Social Sciences) au
Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii au Ustawi wa Jamii au Maendeleo ya
Vijana (Advanced Diploma in Social Works or Community Development or Youth
Development) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serkali.
23.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
24.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
24.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
 Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
 Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
 Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.
 Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
24.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya
Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
24.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
25.0 AFISA ARDHI DARAJA LA II (LAND OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
25.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kusimamia uingizaji wa kumbukumbu katika kompyuta.
 Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria.
 Kufanya ukaguzi wa viwanja.
 Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki kwa visivyoendelezwa kwa
mujibu wa sheria.
 Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi.
25.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Usimamizi ardhi na
Uthamini au Shahada ya Sheria kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali
wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitano.
25.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi
26.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - KOMPYUTA (COMPUTER TECHNICIAN
GRADE II) – NAFASI 1
26.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
26.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani yenye muelekeo wa kompyuta
 Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo
vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya kompyuta
 Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi
kinachotambuliwa na Serikali,
 Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani yenye muelekeo wa kompyuta katika
Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
26.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
27.0 AFISA BIASHARA DARAJA LA II (TRADE OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
27.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kuwasiliana na Wizara nyingine ambazo zinafanya biashara, kupata takwimu
ambazo zitatumika katika kutathimini mwenendo wa biashara na masuala
mengine ya kibiashara.
 Kusambaza taarifa za kibiashara kwa wafanyabiashara.
 Kutathmini mwenendo wa biashara kwa kuangalia hali ya masoko katika nchi
mbalimbali ambazo bidhaa zetu zinauzwa.
 Kuandaa grafu na “chart” ambazo zinaonyesha, mwenendo wa bidhaa
zinazoingizwa nchini na zile ziendazo nje kwa kila nchi ambazo hufanya biashara
na Tanzania.
27.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Biashara waliojiimarisha katika
fani ya Uchumi, Masoko, Uendeshaji Biashara au inayolingana nayo kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salam au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.
27.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
28.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 1
28.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
 Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
 Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
 Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.
 Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
28.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na
NBAA
28.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
29.0 AFISA USIMAMIZI WA FEDHA DARAJA LA II (FINANCE MANAGEMENT
OFFICER II) - NAFASI 1
29.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandikisha na kudhibiti Amana (Securities) za Serikali.
 Kufuatilia hati za hisa.
 Kuwasiliana na watoaji mikopo/misaada kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa
miradi.
 Kuweka kumbukumbu za madeni ya nje.
 Kuweka kumbukumbu za mikopo ya ndani.
 Kufuatilia na kusimamia matayarisho ya makadirio ya mapato na matumizi ya
Serikali.
 Kufuatilia utayarishaji na uchambuzi wa “Flash Reports” za kila mwezi.
29.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya
Uchumi na Mipango (Major in Economics) au Biashara au Sheria (LL.B) au
Stashahada ya Juu ya Uhasibu au Uchumi & Mipango au Biashara au Stashahada
ya juu ya Usimamizi wa kodi kutoka Chuo/Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
 Waombaji wenye Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa nyingine
inayolingana na hiyo inayotambuliwa na NBAA watafikiriwa kwanza.
29.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
30.0 AFISA TARAFA – NAFASI 6
30.1
MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.
 Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali
Kuu katika Tarafa.
 Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata
kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
 Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye
Tarafa.
 Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
 Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
 Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha
kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
 Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
 Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za
maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
 Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
 Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
 Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo
katika eneo lake
 Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
 Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo
lake
 Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa
ushauri.
 Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa
kutoka kwa Watendaji wa Kata.
 Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji,
Manispaa au Jiji.
30.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za
Sheria,Menejimenti,Utawala,Sayansi ya Jamii, Kilimo, Mifugo,Ushirika, Mazingira,
au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
30.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.
31.0 AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II)
– NAFASI 1
31.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa vyuo, shule, na vituo vya Elimu na
Mafunzo
 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa waalimu, Makocha, viongozi wa
vyama na vilabu vya michezo
 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.
31.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo (Physical
Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
31.3
MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
32.0 FUNDI SANIFU DARAJA II – RAMANI (TECHNICIAN GRADE II - (MAPPING) –
NAFASI 1
32.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kushughulikia madaai/malalamiko ya hati za viwanja, kuweka na kutunza
kumbukumbu zake
 Kutunza kumbukumbu za “cadastrals surveys” na mahesabu yake
 Kuandaa nakala za “cadastral site plans”
 Kutunza miongozo ya ramani (maping guides) na viwanja
32.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ramani (Mapping)
32.3
MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
33.0 FUNDI SANIFU DARAJA II- URASIMU RAMANI (CARTOGRAPHY) – NAFASI
1
33.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya maandalizi ya Uchoraji wa ramani za miji kadiri ya uwiano unaohitajika
 Kutunza kumbukumbu za ramani na plan
 Kuchora plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji
 Kutoa nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji
33.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili au Stashahada katika fani ya Urasimu Ramani
(Cartography) kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
33.3
MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
34.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI - (TECHNICIAN GRADE II - WATER) –
NAFASI 1
34.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji
 Kutunza takwimu za maji
 Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye
michoro
 Kuchora hydrograph za maji
 Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post”
n.k.
 Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa
 Kuingiza takwimu kwenye kompyuta
 Kufundisha wasoma vipimo
34.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana
cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa
kutumia kompyuta.
34.3
MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
35.0 AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 1
35.1
MAJUKUMU YA KAZI
 Kutekeleza Kazi za Ushirikishaji Wadau Katika Uhifadhi.
 Kudhibiti Utoaji wa Leseni za Biashara Za Nyara na Vibari vya Kukamata
Wanyama Hai.
 Kushiriki Katika Kusuluhisha Migogoro ya Matumizi ya Wanyamapori
 Kudhibiti Matumizi Haramu ya Leseni za Uwindaji na Kuhahakikisha Kufuatwa
Kwa Maadili Katika Kutumia Wanyamapori.
 Kuthibiti Matumizi Haramu ya Wanyamapori.
 Kufuatilia Utekelezaji wa Miongozo Mbalimbali ya Uhifadhi Wanyamapori.
 Kuhakiki Viwango vya Kukamata Wanyama Hai Kwa Ajili ya Biashara na Ufugaji.
 Kufanya Kazi za Kuzuia Ujangili.
 Kukusanya Taarifa, na Takwimu za Uhifadhi.
 Kutekeleza Kazi za Uhifadhi Katika Mapori ya Akiba.
35.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa Wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori Kutoka Chuo Kikuu
Kinachotambuliwa na Serikali.
35.3
MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi
36.0 AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) – NAFASI 2
36.1
MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili watafanya
kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni pamoja na:
 Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na
Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.
 Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo
ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.
36.2
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
36.3
MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi
X. M. Daudi
Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Read More »

Ya Chopa 3, ushindi Kata 3 na masuala ya msingi kwa wanaCHADEMA, wapenda demokrasia

0 comments

Kuna mambo mengi yamezungumzwa tangu jana na hadi leo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa marudio katika kata 27 na ushindi wa CHADEMA katika kata 3 za Kiborloni, Sombetini na Njombe mjini.

Tutaendelea kusoma, kusikiliza na kupokea kila aina ya criticism, zinazotolewa kwa njia mbalimbali, ingawa hatimaye tutafanyia kazi constructive criticism zinazojengwa katika dhamira ya kweli na nia njema kwa ajili ya mustakabali wa Watanzania na chama chao, CHADEMA.

Moja ya masuala yanayozungumzwa na wapinzani wa CHADEMA, ambayo hata leo katika press conference iliyoitishwa Lumumba, litazungumza sana, ni kujaribu 'kuoanisha' M4C-OPD (matumizi ya chopa 3) na ushindi wa kata 3.

Kuoanisha mambo hayo kwa mgongo wa kufanya uchambuzi au tathmini ya mambo hayo mawili, ni ama kuamua kuwa myopic kwenye hoja muhimu au kuamua kupotosha kwa makusudi ya propaganda nyepesi au kutokujua tu.

Wakati Mwenyekiti Mbowe anazindua M4C- Operesehni Pamoja Daima, mbele ya waandishi wa habari alisema malengo ya shughuli hiyo maalum kuwa itaweka msisitizo au mkazo kwenye masuala makuu yafuatayo;


  • Mchakato wa katiba mpya
  • Daftari la wapiga kura
  • Wazawa na rasilimali za nchi yao
  • Ugumu wa maisha unaosababishwa na uongozi mbovu na sera zilizoshindwa za CCM


Kwa wale waliofuatilia OPD, kila mtu anajua namna ambavyo imeibua mjadala mkali katika masuala hayo, kuanzia na katiba mpya, wazawa na matumizi (unufaikaji) ya rasilimali, ugumu...

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikalazimika kutangaza kwamba tayari serikali imetoa fedha za kuboresha daftari la wapiga kura. Haitoshi tu kusema hivyo. Viongozi wakuu, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Slaa wakatoa kauli ya chama wakiitaka NEC itoe taarifa kamili juu ya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na;

  • Ratiba kamili ya shughuli hiyo
  • Lini NEC itaanza kukagua vituo
  • Tarehe rasmi ya kuanza kuboreshwa daftari
  • Serikali imetoa bajeti ya kiasi gani (inatosha kwa shughuli nyeti kama hiyo?


Kwa sababu M4C-OPD ilikuwa ni ya nchi nzima, yako maeneo ya uchaguzi ambako chopa zilifika. Lakini kuoanisha matumizi ya chopper 3 na matokeo ya ushindi wa kata 3, ni kulazimisha hoja isiyokuwepo kwa premises za kuokoteza.

Wapinzani wa CHADEMA wakisukumwa na euphoria ya ushindi usiokuwa na uhalali (tutafafanua), wamejikita kwenye 'negative (ya picha)' inayozungumzia chopper 3 kwa kata 3, wanashindwa kuiona 'picha kubwa' (negative Vs bigger picture), inayozungumzia masuala kadhaa, mfano;

Katika uchaguzi wa 2010 matokeo yalikuwaje?
Je kuna mabadiliko ya goal post, figures na namba?
Je mabadiliko hayo yako in favour of status quo au yanasapoti vuguvugu la mabadiliko?

CHADEMA itajikita katika hayo kwa sababu ni muhimu sana katika suala kulinda demokrasia ya watu na kusheherekea ushindi, hasa ushindi ulio halali.

Mfano; katika Kata ya Njombe mjini, mwaka 2010 CHADEMA haikusimamisha mgombea kabisa wa udiwani wala ubunge. Mgombea Urais wa CHADEMA alimzidi kwa mbali mno mgombea urais wa CCM. Mbali mno.

Matokeo ya jana katika kata hiyo hiyo kwa uchaguzi wa udiwani, yanaonesha kwamba;



CHADEMA imepata kura 2,202

CCM imepata kura 1,094

Jumla ya kura zilikuwa 3334

Jumla ya vituo vilikuwa 41, CCM imeshinda kituo kimoja tu kwa tofauti ya kura 9

Iko mifano mingi ya namna hii katika uchaguzi wa jana. Kuna maeneo ambayo CHADEMA haikuwahi kuweka mgombea, imetoa ushindani mkali na kuna maeneo ambayo uchaguzi uliopita kulikuwa na tofauti kubwa mno ya kura, lakini safari hii gap limepunguzwa kwa namba kubwa sana.

Mfano Kata ya Mpwayungu, Mtera, Dodoma

Mwaka 2010

CHADEMA 602
CCM 1812

Mwaka 2014 (jana)

CHADEMA 555
CCM 872


Katika Kata ya Ubagwe, mwaka 2010, CCM ilipita bila kupingwa. Uchaguzi wa jana umekuwa;

CCM 329
CHADEMA 215
TADEA 71
Zilizoharibika 3

Where are the voters? Where is legitimacy?

Moja ya masuala ya msingi sana ambayo tulitarajia yawaumize kichwa sana watu, hususan walioko madarakani ni swali hili; Je wapiga kura wako wapi?

Suala hili limepewa uzito na CHADEMA pamoja na wapenda demokrasia na maendeleo wengine wengi tu nchini tangu baada tu ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Nani anajali?

Walioko madarakani wangelikuwa wanathamini mchakato wa demokrasia ya uwakilishi, ambayo maana yake ni kuwaheshimu watu/wapiga kura, kamwe wasingekuwa wanakimbilia kushangilia matokeo, tena yasiyowapatia uhalali.

Mathalani

Kata ya Ubagwe, Ushetu, Shinyanga

Wapiga kura walioandikishwa wako 4270

Waliopiga kura jana ni 618

CCM wameshinda kwa kura 329 dhidi ya CHADEMA kura 215, TADEA- 7, zilizoharibika 3.

Kata ya Nyasura Bunda,

Waliojiandikisha ni 5333
Waliopiga kura 1579

Wapiga kura wako wapi? Uko wapi uhalali wa washindi?

Aidha, wapinzani wa CHADEMA hawataki kabisa kabisa kuzungumzia irregularities. Hawataki kabisa kugusia namna ambavyo watu wamepigwa wazi wazi na kuchukuliwa kwenye vituo vya kura, wakiwemo mawakala wa CHADEMA kisha eti wakapelekwa vituo vya polisi.

Wapenda demokrasia hao ya ushindi, hawataki kabisa kuzungumzia mapanga na mashoka yaliyotembezwa jana na Green Guards!

Huwezi kuzungumzia kushindwa au kushinda kwenye matokeo ya jana au mengine yoyote yale, bila kujadili masuala hayo kwa upana sana, unless kama tumekubaliana kuwa iwe ni sehemu ya demokrasia yetu, watu kukatwa mapanga, mashoka, damu kumwagika, watu kukamatwa vituoni bila makosa, kisha CCM wakaachwa wanafanya wanavyotaka, wakuu wa wilaya kuingia vituoni na kutoa maagizo.

Labda kwao ni sehemu ya mchakato wa kuchagua wawakilishi! Vinginevyo basi tuanze kuwaandaa Watanzania kwa uchafu wa namna hii.

Kwa kusema haya kamwe haimaanishi kuwa CHADEMA haihitaji kufanya tathmini ya kitaalamu, kitaaluma na kina sana. Itafanyika na itakuwa muhimu kwa ajili ya kuendelea kujiimarisha na kujipanga katika mapambano haya.

Lakini kwa vyovyote ni muhimu sana sana, kuweka mikakati ya kukabiliana na Intarahamwe inayotaka kupandikizwa Tanzania na Watawala dhidi ya Watanzania.

Suala hili la Green Guards kufanya maovu dhidi ya wapinzani wa CCM kwenye uchaguzi, tena mahali pengine uovu wa kutisha unaohusisha silaha, kwa namna ile ile ya Intarahamwe, mbele ya askari polisi, wala wasiguswe, wapo wengine bado wanaliona kuwa ni jambo dogo au mzaha fulani hivi.

Siku madhara yake yatakapokuwa yameshafika mfupani, tutajua Intarahamwe ilikuwa ni kitu gani, kilianzaje, kilipataje nguvu na matokeo yake yalikuwa ni nini.

Where are the voters, where is legitimacy?

Makene


Read More »

UKUMBI WA BUNGE LA KATIBA: Sekretarieti ya Bunge la Katiba kukabidhiwa Ukumbi Jumatano

0 comments






Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akijaribu mojawapo ya viti vipya vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge tayari kwa ajiri ya Matumizi wakati wa Bunge la Katiba. Mhe. Makinda aliongoza ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Bnge kufanya ukaguzi wa mwisho kabla ukumbi huo haujakabidhiwa kwa Sekretariat ya Bunge la Katiba Jumatano wiki hii.

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kukagua ukumbi huo.

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda, (katikati) Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (kushoto), Katibu wa Bunge (Wa pili Kulia) na Mhe. Hamadi Rashid Mohamed Kulia wakiangalia baadhi ya maboresho yaliyofanywa katika Ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Bunge la Katiba.


Muonekano wa Ndani ya ukumbi huo baada ya kazi ya uwekaji viti kukamilika.

Mojawapo ya viti maalum vilivyowekwea katika ukumbi huo kwa ajili ya matumizi ya watu wenye ulemavu.


Viti vyote vipya vina nembo ya taifa.

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda pamoja na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi walioshiriki kuukarabati ukumbi wa Bunge kwa ajiri ya matumizi ya Bunge la Katiba.
Picha kwa hisani ya Bunge.


Read More »

Waziri wa uhamiaji wa Uingereza ajiuzulu

0 comments
Mark Harper
Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.
Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.
Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.
Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu

Read More »

Malumbano CCM: Kiyabo amjibu Makonda

0 comments
 
MALUMBANO ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanayoonekana dhahiri kuchagizwa na makundi ya urais yameendelea kushika kasi ndani ya chama hicho.

Baada ya jana Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda, kumshambulia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kwamba anawatumia watu kusema hovyo kupitia vyombo vya habari juu ya kazi na juhudi zinazofanywa na sekretarieti, kada mwingine, Richad Kiabo, jana aliibuka kuanika majina ya waasisi wa chama cha siasa cha CCJ kilichokufa hata kabla ya kupata usajili.

Makonda alidai Lowassa anafadhili mikakati ya kupingana na juhudi za sekretarieti ya chama hicho na alipongeza kazi zinazofanywa na sekretarieti chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana na wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, akijibu mapigo ya Makonda, Kiabo aliyekuwa mwenyekiti wa CCJ kabla ya kurejea CCM, aliyataja majina 37 na michango waliyoitoa kwa ajili ya kufanikisha maandamano ya amani ya chama hicho ya kupinga uonevu wa aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa nchini wakati huo, John Tendwa.

Kiabo ambaye amekoleza malumbano hayo, alimtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, kuwachukulia hatua wasaliti hao.

Mbele ya waandishi wa habari, Kiabo aliwataja waasisi hao wa CCJ na fedha walizochangia kwenye mabano kuwa ni pamoja na Dk. Harrison Mwakyembe (sh 300,000), Samuel Sitta (sh 500,000), Anne Kilango (sh 400,000), Nape Nnauye (sh 100,000), Paul Makonda (sh 100,000) na James Lembel (sh 400,000) ambao kwa sasa ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwa na makundi ya urais.

Wengine ni Amina Katemi (sh 300,000), Alex Kisumo (sh 300,000), Baraka Seif (sh 300,000), Sospeter Banigwa (sh 300,000), Saleh Omari (sh 300,000), Sarah Patrick (sh 200,000), Daniel Mwaijojeli (sh 200,000), Dk. Ngonyani (sh 300,000), Elisha Eliya (sh 200,000), Emanuel Magonja (sh 200,000) na Asma Watosha (sh 300,000).

Pia wamo, Kulwa Lulelema (sh 50,000), Hamadi Maduku (sh 100,000), Flavian Nkya (sh 100,000), Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000), Hamad Ferej (sh 200,000), Ally Harun (sh 50,000), Masudi Kangi (sh 100,000), Gumbo (sh 150,000), Idd Kiriwe (sh 100,000), Innocent Makala (sh 200,000), Jacob Msambya (sh 200,000), Ishelula (sh 150,000), Kipute (sh 200,000), Joseph Kashindye (sh 200,000) Kamala Ng’ombe (sh 200,000) na Daniel Malongo (sh 50,000).

Kiabo alisema anashangaa kuona ndani ya CCM bado kuna wanachama na viongozi waandamizi wenye kadi mbili, yaani kadi ya CCJ na CCM na wameshindwa mpaka sasa kuzirudisha na hata kukana, ikiwemo kuwaomba radhi wanachama kwa kitendo cha usaliti.

“Nawashangaa baadhi ya wanachama ambao si waaminifu na wasaliti wa chama baadhi yao wameanza harakati za kugombea urais 2015 ili wapewe ridhaa na chama ambacho tayari walikwisha kisaliti, nami nitakishangaa chama wakati ukifika kama kitawakubalia na kuwapitisha kuwa wagombea watu wenye kadi za vyama viwili,” alisema.

Kiabo alisema watu wenye uwezo wa kuwasema viongozi wenzao mara kwa mara na wao wasijisahau kuwa hawana usafi wowote wa kusema na kuwanyoshea vidole wenzao kwa usaliti walioifanyia CCM.

Aidha, alisema wakati CCM ikielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015 ni vizuri kikaanza kusafisha nyumba yake ili mamluki waumbuke na wasipewe nafasi ya kugombea wakati ukifika.

Kutoka jijini Morogoro, inaripotiwa kuwa UVCCM Mkoa wa Morogoro imemtaka Makonda kumwomba radhi Lowassa kwa kauli za kichochezi zinazoweza kukigawa chama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii jana, wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia kundi la vijana, Jonas Nkya na Ramadhani Kimwaga, walisema kauli ya Makonda ni yake binafsi wala haihusiani na UVCCM.

Nkya alisema vijana wa Mkoa wa Morogoro wamehuzunishwa na matamshi ya Makonda akimshutumu Lowassa kuwa hafai kuwa kiongozi wa nchi hii, wala kuwa Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa CCM taifa.

Nkya alisema kuwa umoja huo hautaki kuingizwa katika masuala binafsi ambayo yanaweza kusababisha na kuchangia kukigawa chama na jumuiya zake.

Mnyukano wa sasa miongoni mwa makada wa CCM umekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri na kuwarejesha madarakani mawaziri mizigo waliopendekezwa na chama chake watoswe.

Baada ya uteuzi huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alitoa kauli ya kuunga mkono uteuzi huo, lakini akisisitiza chama kitaendelea kuwashughulikia mawaziri mizigo na safari hii wataelekeza mapambano hayo ndani ya Bunge na kwenye mabaraza ya halmashauri.

Kauli hiyo ilimuibua mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, ambaye alimtukana Nape kwamba ameteuliwa kimjombamjomba na hawezi kumchagulia rais majina ya uteuzi.

Kauli ya Guninita ikamuibua Makonda na sasa Kiabo, ambao duru za siasa zinasema wote wamepewa hela kwa malengo ya urais mwaka 2015

Read More »

Abiria 17 akiwemo waziri wa katiba na sheria wamesalimika kifo baada ya ndege kufeli breki

0 comments
 
Abiria 17 akiwemo waziri wa katiba na sheria Zanzibar Mhe. Abubakari khamis bakar, na marubani wawili, wamesalimika kifo baada ya ndege ya shirika la ndege la ‘Zanz air’ kufeli breki, muda mfupi wakati ndege hio ilipo kuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Abeid amani karume, uliopo nje kidogo ya mji wa chakechake mkoa wa kusini Pemba
Kwamujibu wa tarifa zilizo tolewa na makamanda wa polisi mkoa kusini Pemba kamishina msaidizi swalehe mohamed swalehe na kamanda wa kikosi cha zima moto na uokozi pemba wamesema ndege hiyo wakati wa kutua ilipata ikhitilafu ya kufeli breki na kusereka hadi nje ya uwanja umbali wa mita miambili kwenye vichaka

Wamesema abiria wote wametoka salama hakuna alie juruhiwa licha ya ndege hio kuacha uwanja kusereka kwenye nyasi na kungia kwenye mashamba ya muhogo kupita kwenye masiki majiti yalio katwa nakisha kusimama baada ya ringi kujizonga namizizi ya pori hilo.

Ipo haja kwa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kutoa taluma kwa watendaji wa kiwanja cha ndege kisiwani pemba kutoa ushirikiano kwa wandishi wa habari pale inapo tokea dharura kutokana na watendaji wa kiwanja chandege kisiwani hapa kushindwa kabisa kutoa usjhirikiano kwa wandishi juu ya tukio hili.

Read More »

CHADEMA yawasilisha pingamizi dhidi ya Zitto

0 comments





Click image for larger version. 

Name: tundu-kibatala-jan24-2014(1).jpg 
Views: 0 
Size: 84.7 KB 
ID: 134195 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewasilisha majibu na pingamizi la awali dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuhusu Kamati Kuu ya Chama hicho akiitaka mahakama kuzuia uanachama wake usijadiliwe hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.

Kadhalika, chama hicho kimejibu barua ya Zitto pamoja na kuwasilisha mwenendo wa shauri lililopelekea kuvuliwa nyadhifa za uongozi katika chama hicho kama mlalamikaji alivyoomba.

Majibu hayo yaliwasilishwa jana Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Mawakili wa chama hicho, Tundu Lissu na Peter Kibatala, katika pingamizi hilo kuna hoja sita na wakiitaka Mahakama kutupilia mbali kesi hiyo kwamba haina mashiko ya kisheria.

Hoja hizo ni shauri hilo halina msingi kwa sababu halikuwasilishwa katika Mahakama ya chini kusikilizwa na kutolewa maamuzi kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha Mwenendo wa Mashauri ya Madai.

Limewasilishwa masijala Kuu ya Mahakama Kuu badala ya masijala ya Wilaya kinyume cha sheria na taratibu za masijala za Mahakama.

Mlalamikaji hajaomba maoni ya Mahakama Kuu kuhusiana na suala linalohusiana na uanchama wake Chadema.

Nyingine ni shauri halina msingi kwa sababu Zitto anaendesha mashauri mawili, Mahakama Kuu na rufaa ya kwenye Baraza Kuu la chama.

Pia Mahakama Kuu siyo mahali pake kwa sababu Zitto hajatumia nafasi zilizopo ndani ya Chadema.

Mahakama Kuu haina mamlaka ya kutoa maamuzi ya maombi ya kuzuia Zitto asijadiliwe uanachama wake kwa sababu ni mambo ya yanayohusu Chadema.

Chadema wakijibu maombi ya msingi ya Zitto kupitia hati iliyosainiwa na Sylvester Masinde na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, wamedai kwamba hawana ubishi kwamba mlalamikaji alivuliwa uongozi Novemba 22, mwaka 2013.

Pia, inaeleza kwamba Zitto alishiriki katika Mkutano wa Kamati Kuu na alijua kinachoendelea kuhusu tuhuma zake.

Chadema inaomba Mahakama kutupilia mbali maombi ya mlalamikaji kwa kuwa hayana mashiko ya kisheria.

Mapema Januari 2, mwaka huu Zitto kupitia Wakili Albert Msando, alifungua kesi mahakamani hapo dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Dk. Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Mahakama iliyokaa chini ya Jaji John Utamwa ilikubali na kutoa zuio la muda hadi kesi ya msingi itakapoisha.


Read More »