Nyota wa zamani wa Bayern Munich ajitangaza kuwa Bwabwa.
Nyota wa zamani wa Ujerumani Thomas Hitzlspergeraliyeanzia soka lake kwenye klabu ya Bayern Munich amejitangaza kuwa bwabwa.
Nyota
huyo aliwahi kucheza kwenye ligi ya England kwa muda wa miaka mitano
akicheza kwenye klabu ya Aston Villa kabla ya kujiunga na VFL Stutgart
ya nyumbani kwao ujerumani ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa ligi ya
Ujerumani Bundesliga.
Thomas
pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya
kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 ambako alicheza
mechi zote za hatua ya mtoano kuanzia robo fainali , nusu fainali na
fainali.
Kiungo huyu mshambuliaji pamoja na kuwa raia wa
Ujerumani alichea sehemu kubwa ya soka lake nchini England kwenye timu
za Aston Villa, West Ham United na Everton pamoja na Stuttgart, Bayern
Munich alikoanzia soka lake na Werder Bremen. Moja ya vitu ambavyo
Hitzlsperger atakumbukwa navyo ni mashuti makali aliyokuwa anapiga kwa
mguu wake wa kushoto na alifunga mabao mengi sana kwa style hiyo.
Kiungo huyu alistaafu kucheza soka mwaka jana akiwa
na umri wa miaka 31 baada ya kuandamwa na majeraha tofauti ya goti kwa
muda mrefu.
Thomas
Hitzlsperger anakuwa mchezaji wa pili maarufu kujitangaza kuwa shoga
baada ya mchezaji wa zamani wa Leeds United Robbie Rogers ambaye kwa
sasa anacheza kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy naye kujitangaza kuwa
shoga.
0 comments: