RATIBA ya M4C - Operesheni Pamoja Daima: Kigoma, Rukwa, Mbeya, Manyara na Arusha

0 comments
 
Ratiba ya leo itakuwa kama ifuatavyo;

Timu ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Issa Mohamed, John Mnyika na

Uvinza- (Nguruka), Kigoma Kaskazini- (Mikongolo na Kagunga), Kigoma mjini

Timu ya Katibu Mkuu Dkt. Slaa;

Mbeya Vijijini (Santilya), Vwawa, Nkasi (Kasanga) na Sumbawanga mjini

Timu ya Tundu Lissu na John Heche;

Moshi Vijijini (Mabogini), Mererani, Ngarenanyuki na Sombetini (kata ya uchaguzi)

Hii ndiyo ratiba rasmi ya leo, ikionesha kiongozi gani atakuwa mahali gani.

Read More »

Dr Slaa afunika Songea wana nchi wamsikiliza bila kujali Mvua

0 comments



 
       Dr Slaa Akimwaga Cheche

          Wananchi wakimsikila za mvua
KATIBU MKUU wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbroad Slaa amesema kuwa rasilimali za Tanzania zinapaswa zilindwe na watanzania wenyewe na sio kuwaachia wageni kutoka nje kama ilivyo hivi sasa serikali ya chama tawala imekuwa ikwaachia mafisadi ambao wamekuwa wakishirikiana na wageni kuziamisha rasilimali za watanzania.
Dr. Slaa ameyasema hayo leo kwenye mkutano mkubwa uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa manispaa ya Songea kwenye viwanja vya shule ya msingi Matarawe ambako aliwaeleza wakazi wa Songea kuwa taifa la Tanzania kwa zaidi ya miaka hamsini serikali ya chama cha mapinduzi imeshindwa kusimamia rasilimali hizo na ndio maana inaonekana wanaonufaika nazo ni wachache.

Katika mkutano huo ambao ulizingirwa na mvua kubwa katibu mkuu huyo Dr Slaa aliendelea kuwahutubia wananchi kwa kutoa mfano mkoa wa mtwara kuwa na machimbo ya gesi lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida rais Jakaya kikwete aliamuru kupeleka askari wa jeshi la wananchi kwenye maeneo hayo wakati nia ya serikali yake imeonekana kuwa na lengo la kuwakaribisha wawekezaji wageni badala ya wawekezaji kutoka ndani ya nchi.

Wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha huku akiendelea kuhutubia mkutano huo Dr Slaa alieleza kuwa pamoja na kuwa viatu vyake vimejaa maji kutokana na kunyeshewa na mvua hiyo alisema kuwa hawezi kusitisha mkutano huo mpaka kieleweke ambapo aliwataka wananchi wa Songea waone umuhimu wa kuacha itikadi za vyama na dini ili kujenga uchumi wan chi kwa kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi ikiwemo gesi zisimamiwe na watanzania wenyewe na si vinginevyo.

Mapema mbunge wa Iringa mjini kupita CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa serikali ya CCM hailingani kabisa na umri wa miaka hamsini tangu nchi ya Tanzania ilipopata uhuru kwani rasilimali zilizopo haziwasaidii watanzania badala yake wanyama kama twiga, faru na wanyama wengine wenye kuliletea tija taifa wamekuwa wakisafirishwa kuuzwa nchi za ulaya wakati vyombo vya ulinzi vipo ikiwemo idara ya usalama wa taifa.

Aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye serikali za mitaa, vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na kuhakikisha kuwa wananchi wanaipigia kura CHADEMA kwa nguvu zote na kuicha CCM ikiwa mbendembende.

Ameshangazwa sana serikali ya CCM ambayo imekuwa ikiendelea kuwabeba mawaziri ambao CCM yenyewe kupitia katika wa itikadi na uenezi bwana Nape Mnauye na katibu mkuu wa ccm bwana Abdalla Kinana ambao wamedaiwa kuwa ni mizigo ndani ya serikali lakini mwenyekiti wao ambaye ndiye rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete ameamua kuwarejesha kwenye baraza la mawaziri wakati kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikiwa na watanzania.

Read More »

John Mnyika:UFAFANUZI KUHUSU UPANUZI NA MGOGORO KUHUSU UPANA WA BARABARA YA MOROGORO

0 comments

Kwa nyakati mbalimbali kati ya mwaka 2004 na 2013 nimezungumzia haja ya upanuzi wa Barabara ya Morogoro kutoka Jimboni Ubungo kupitia Kibaha mpaka Chalinze na mgogoro uliodumu muda mrefu kuhusu upana wa Barabara hiyo.

Ningependa kutoa ufafanuzi kwamba nyakati zote nimeunga mkono upanuzi wa Barabara hiyo ikiwemo ujenzi wa barabara hiyo kuwa njia sita (tatu kwenda na tatu kurudi).

Hata hivyo, mara nyingi nimekosoa masuala manne kuhusu upanuzi na mgogoro kuhusu upana wa barabara ya Morogoro:

Mosi, Serikali kutoa ahadi bila utekelezaji kwa miaka mingi. Mwaka 2012 na 2013 Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli amekuwa akirudia kauli kwamba ujenzi wa Dar Es Salaam-Chalinze express road kuanza. Katika mkutano wangu na wananchi jimboni tarehe 19 Januari 2014 kuhusu ujenzi wa Barabara hiyo, nimesisitiza kwamba fedha za ujenzi wa barabara hiyo hazijatengwa hivyo ujenzi hauwezi kuanza. Badala yake nilifafanua kwamba Serikali inachokifanya kwa sasa ni kutafuta mkandarasi mwenye uwezo wa kutafuta fedha na kujenga. Hivyo, ni muhimu Serikali ikawaeleza wananchi ukweli na kuharakisha kutekeleza ahadi zilizotolewa kwa miaka mingi.

Pili; badala ya Serikali kuja na wazo la kujenga njia zaidi ya 6, ianze kwanza kutekeleza ahadi ya njia hizo sita; kwa kuanza na ujenzi katika umbali wa mita 60 zilizopo. Hivyo, sioni haja ya Serikali kujenga kwa sasa mpaka eneo la upana wa mita 241 wakati ambapo kuna barabara nyingine muhimu za pembezoni ya Barabara ya Morogoro ambazo zikiharakishwa kujengwa zinaweza kupunguza foleni mf. Barabara ya Goba-Mbezi-Msigani-Malambamawili-Kinyerezi na nyinginezo ambazo ujenzi wake unasuasua.

Tatu; Serikali kupotosha kwa miaka mingi kuhusu upana wa barabara hiyo. Mwaka 2011, 2012 na 2013 Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli amekuwa akidai kwamba upana wa barabara hiyo unahusisha pia maeneo yenye upana wa mita 242 ( mita 121 kutoka katikati ya barabara kwa kila upande) kuanzia Jimboni Ubungo hadi Kibaha; na kwamba wananchi wanaoishi katika maeneo ya ndani ya upana huo ni wavamizi wasiostahili kulipwa fidia. Kwa nyakati mbalimbali nimepinga kauli hiyo ya Waziri na yamekuwepo malumbano kuhusu suala hilo. Mara zote nimesisitiza kwamba upana wa barabara hiyo ni mita 60 (yaani 30 kwa kila upande kutoka katika kati ya barabara). Hivyo, wakazi katika eneo hilo hawajavamia barabara na wamehamia kihalali kwa msukumo wa Serikali kuanzia wakati wa Operesheni vijiji ya mwaka 1970.

Mkutano wangu na wananchi wa tarehe 19 Januari 2014 ulijadili suala hili kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kupitia shauri Na 80 la 2005 na kutoa hukumu tarehe 31 Mei 2013 ambayo pamoja na mambo mengine imetamka kuwa The Highway Ordinance Cap 167 Government Notice No 161 of 5/5/1967 ambayo hutumiwa na Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuingia katika ardhi za wananchi “ni batili kwa kutofautiana na vifungu vya 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji na 5 ya 1999”.

Tatu; kwa nyakati zote nimesisitiza kwamba iwapo Serikali inataka kutwaa maeneo ya nyongeza kwa ajili ya ujenzi nje ya nafasi ambayo tayari inawezesha ujenzi wa barabara hiyo basi Serikali ihakikishe inalipa kwanza fidia kwa wananchi kabla ya kubomoa nyumba za wananchi na kuwasababishia umaskini. Suala hili nalo nililisisitiza katika mkutano wangu na wananchi tarehe 19 Januari 2014 katika eneo la Luguruni.

Hivyo, habari iliyoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima 21 Januari 2014 (uk 2) kwamba Mnyika “alisema haoni ya kupanua barabara kutoka Kibaha hadi Dar es Salaam wakati maeneo mengine ya nchi hayana barabara zinazopitika kwa kirahisi” si sahihi.

Aidha, kauli ya Wakala wa Barabara (TANROADS) kupitia Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar Es Salaam Julius Ndyamkama kwamba “watu waliojenga kinyume cha sheria ndani ya hifadhi ya barabara pembezoni mwa barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo hadi Kibaha wamekuwa wakidaganyana kuwa nyumba zinatakiwa kuwa umbali wa mita 30 kutoka barabarani, lakini ukweli ni kwamba nyumba zinaruhusiwa kujengwa umbali wa mita 121 kutoka katika barabara za TANROADS” nayo sio sahihi.

Katika muktadha huo, namshauri Rais Jakaya Kikwete kukaa na mawaziri wake kuwaelekeza kuipitia, kuiheshimu na kuwezesha utekelezaji wa maamuzi ya mahakama pamoja na kuharakisha ujenzi wa barabara huku ikilinda haki za msingi za wananchi wa majimbo ya Ubungo, Kisarawe, Kibaha Mjini na Chalinze walioshi pembezoni mwa barabara hiyo wenye haki zilizotambuliwa tangu wakati wa Operesheni Vijiji.

Kadhalika, badala ya kuendeleza malumbano Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli na Watendaji wake wa Wakala wa Barabara (TANROADS) waelekeze nguvu za haraka katika kusimamia ujenzi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka (BRT) ambapo Mkandarasi (Starbag) na Wakala (DART) hawatekelezi ipasavyo masharti ya mikataba.

Masharti hayo yanayokiukwa na ni pamoja na kushindwa kuweka njia mbadala za kutosha na alama inavyostahili na hivyo kusababisha msongamano mkubwa katika barabara ya Morogoro wenye athari kwenye uchumi wa nchi na kuleta usumbufu kwa umma.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
21/01/2014

Read More »

Ratiba ya M4C- Operesheni Pamoja Daima, Ruvuma, Tabora na Tanga

0 comments

 
Kama ambavyo jana umma wa Watanzania ulitaarifiwa kupitia kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na wanahabari, Chama leo kinaanza operesheni ya takriban wiki mbili kwa nchi nzima (mijini na vijijini).

Kuna jumla ya timu 6 zilizoko uwanja wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni Pamoja Daima, ambazo zote zinaanza kazi leo katika maeneo zilizopangiwa. Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.

Timu hizi zinajumuisha viongozi wakuu wa Chama, watendaji kutoka Makao Makuu ya Chama, Wajumbe wa Kamati Kuu, Viongozi wa Kanda, Mikoa, Wilaya, Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji pamoja na wabunge wote wa CHADEMA katika maeneo husika.

CHADEMA itatumia operesheni hii ya wiki mbili kuandaa umma wa Watanzania juu ya masuala kadhaa muhimu kwa hatma ya nchi yao;

1. Mjadala wa rasimu ya pili ya katiba mpya- Bunge Maalum la Katiba Mpya
Wakati huu ambapo nchi Watanzania wanasubiri vikao vya Bunge Maalum la Katiba,
pamoja na Tume ya Warioba kufanya kazi nzuri kwa kukusanya na kuzingatia
maoni ya watu (ambayo CCM wanayapinga wakiweka mbele maslahi ya chama
chao badala ya Watanzania wenye nchi yao), bado kuna masuala ambayo;

(a) yanahitaji msisitizo yaendelee kubakia kwenye rasimu

(b) yanahitaji kuboreshwa

(c) yanahitajika kuongezwa kwa sababu hayamo

2. Kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni kuamua
Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Hii ni moja ya shughuli ya 'kufa na kupona' mwaka huu kwa sababu kuna
mamilioni ya Watanzania hadi sasa Serikali ya CCM imewanyima haki yao ya
kikatiba ya kufanya maamuzi yanayohusu maisha yao, maendeleo yao kupitia kura.

3. Uchaguzi wa ndani ya chama ambao hadi sasa unaendelea katika ngazi ya msingi
nchi nzima hatimaye ngazi ya taifa.

4. Masuala ya Watanzania na umiliki wa rasilimali zao ambazo kwa sasa zinaonekana
kuwanufaisha wageni, watawala na watu wenye mahusiano na watawala, pia hali
ya ugumu wa maisha inayozidi kuwakabili wananchi ikiwa na uhusiano na uongozi
mbovu unaokumbatia ufisadi na sera zilizoshindwa, yatapewa kipaumbele kikubwa
katika ziara hii.

5. Bila kusahau kwamba 'all politics is local', hivyo chama kitatumia fursa hii
kuzungumza na wananchi juu ya kero mbalimbali zinazowakabili na CHADEMA
inaweza ku-offer nini. Na mengine kadha wa kadha yenye umuhimu kwa
maendeleo ya watu.

Ifuatayo ni ratiba ya leo na kesho kwa timu tatu za angani ambazo zinatumia usafiri wa helkopta 3;

Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa;

Mbambabay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo kisha kwa leo watamalizia Songea Mjini

Timu ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Issa Saidi Mohamed

Nzega (Ndala), Igunga (Nkinga), Tabora Kaskazini (Mabama) na Tabora mjini

Timu ya Kamanda Tundu Lissu na John Heche

Lushoto, Korogwe, Muheza na Tanga mjini

* Tutawapatia updates kadri muda unavyokwenda. Accounts za CHADEMA mitandaoni ikihusisha pia 'vyombo' vya chama kama websites na blogs, ndizo zitakuwa vyanzo rasmi vya taarifa za uhakika kwa kila kinachoendelea field.

Tutashirikiana na mods pamoja na watu wengine wote hasa walioko fields kwenye timu zote 6 kuhakikisha Watanzania wanapata taarifa sahihi, za uhakika, kwa wakati, huku pia tukiomba uvumilivu wenu na subira inapolazimika, ili kupata vitu vizuri maana mikutano itafanyika maeneo ya vijijini na mijini.

Punde tutatoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za watu kama vile, kwa nini helkopta (tena idadi imeongezeka, hakuna chama cha siasa kiliwahi kufanya kama hivi kwenye operesheni kama hii), kwa nini PAMOJA DAIMA (wengine wanafikiri ni tofauti na M4C).

Haya karibuni kwa ajili ya M4C- PAMOJA DAIMA hii ndiyo habari yenyewe kwa sasa.

Read More »

BREAKING NEW ZZZZZZZZZ Mbunge wa Chalinze (Said Bwanamdogo) afariki dunia

0 comments
Click image for larger version. 

Name: download (2).jpg 
Views: 0 
Size: 3.5 KB 
ID: 133696



Mbunge wa Chalinze (CCM) Mh. Said Bwanamdogo amefariki Dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Mifupa MOI, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu, Ofisi ya Bunge inaendelea na Taratibu za mazishi/maziko baada ya kuwasiliana na ndgu wa marehemu



Read More »

Mwanamke auawa kinyama

0 comments
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Agnes Peter amefariki dunia baada ya kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na watu wasiojulikana na kisha kuondoka na titi lake la kushoto.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Leonard Paul, tukio hilo lilitokea Januari 18 mwaka huu saa 1:30 jioni katika Kitongoji cha Kilobe, Kkijiji cha Namsega, Kata ya Runzewe Magharibi, wilayani Bukombe.
Kamanda Paul alisema kuwa mwanamke huyo mkazi wa Namsega alifariki dunia papo hapo baada ya kukatwa mapanga  sehemu mbalimbali za mwili wake na wauaji hao kuondoka na titi lake la kushoto.
Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo inasadikiwa kuwa ni mgogoro wa muda mrefu wa madai ya fedha uliokuwepo baina ya marehemu na mdai wa fedha hizo ambaye hajulikani alipo.
“Hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuwa mdai wa marehemu huyo alitoweka kusikojulikana na jeshi linaendelea na msako,” alisema.
Kamanda Paul aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo

Read More »

Kipanya LEO

0 comments

Read More »

Picha Maalum Kutoka IKULU Rais Jakaya Kikwete amewaapisha mawaziri saba na manaibu waziri 11 kati ya mawaziri 8 na manaibu waziri 13 aliowateua hivi karibuni katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es salaam.

0 comments

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ikulu jijini Dar es salaam jana . Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akila kiapo
 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria
 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb) Waziri wa Maliasili na Utalii akila kiapo
 Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo
Rais Kikwete akimuapisha  Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha
 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akila kiapo
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo
 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati) akila kiapo
 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji
 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akila kiapo
 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akila kiapo
 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika akiapishwa
 Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo
 Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo
  Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri na manaibu waziri baada ya hafla ya kula viapo
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri baada ya kiapo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
 Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia ya Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria
  Rais Kikwete na familia ya Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb) Waziri wa Maliasili na Utalii 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
 Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia wa  Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati)
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii 
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiwa na baadhi ya mawazir na naibu waziri waliokula kiapo jana
  Rais  Kikwete na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa na makamanda na viongozi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 Rais Kikwete na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani wakiwa na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani
 Rais Kikwete akiongea na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani na wakuu wa vyombo mbalimbali vya dola vilivyo chini ya wizara ya mambo ya ndani
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa na viongozi wa vikosi mbalimbali vilivyo chini ya wizara yake
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya fedha. PICHA NA IKULU.

Read More »